Hivi ndivyo maziwa hayo yanavyoonekana kwa sasa |
Kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited imewapongeza wateja wake kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutumia bidhaa zake .
Afisa masoko wa kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd ya mkoani Iringa Bw Jimy Kiwelu alisema hayo leo wakati akitoa salam za mwaka mpya 2015 na kutambulisha mwonekano mpya wa kisasa zaidi wa chupa za maziwa ya kampuni hiyo kwa sasa.
Alisema mbali ya mafanikio makubwa ambayo kampuni hiyo imefanikiwa kuyafikia kwa kuendelea kupata tuzo ya ubora wa maziwa kwa miaka takribani miwili sasa bado kampuni hiyo imejipanga kuporomoka katika ubora na katika kuhakikisha wanaendelea kushikilia nafasi ya kwanza na ubora wa maziwa nchini Tanzania hivi sasa tayari kampuni hiyo imekuja na mwonekano mpya wa maziwa yake kwa kuwa katika chupa tofauti na zile za mwanzo .
Furaha ya bidhaa mpya ya asas Dairies Ltd katika mwonekano mpya |
Hata hivyo alisema kuwa kuanzisha mwonekano mpya wa chupa za maziwa hayo kumekwenda sambamba na kuongeza ubora zaidi wa bidhaa hizo hivyo kuwakata watumiaji wa bidhaa zao kuanza kufurahia kuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 kwa kutumia maziwa yenye mwonekano tofauti na ule wa mwanzo .
Mwonekano wa zamani
Pia alisema kampuni yake imekuwa mbele katika kuchangia maendeleo ya mkoa wa Iringa kama sehemu ya kutambua ushirikiano mkubwa wa kampuni kwa maendeleo ya Taifa .
Kiwelu alitaja moja kati ya shughuli ambazo kampuni imepata kusaidia kuwa ni pamoja na kuhamasisha jamii ya Iringa na watanzania kupenda kunywa maziwa kwa afya badala ya kutumia muda wao kuingiza sumu mwilini kwa kunywa pombe pia kampuni imepata kutoa msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.7 kwa shule za msingi tatu ambazo zilishinda katika mashindano ya uchoraji wa picha zinazoelezea umuhimu wa unywaji maziwa mashuleni
Mbali ya zawadi hizo kwa shule hizo tatu pia kampuni hiyo ilipata kuwanywesha maziwa wanafunzi zaidi ya 30,000 wa shule za msingi katika Manispaa ya Iringa.
Shule hizo zilizopatiwa msaada wa madawati ni pamoja na Hoho iliyoshika nafasi ya kwanza na kupata madawati yenye thamani ya Tsh milioni 1 ,Mlangali iliyoshika nafasi ya pili na kupata madawati ya Tsh.750,000 pamoja na St Dominic iliyopata madawati yenye thamani ya Tsh 500,000.