Sunday 28 December 2014

KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS YABORESHA ZAIDI HUDUMA ZAKE

Hivi ndivyo  maziwa  hayo  yanavyoonekana kwa  sasa 
                                               Na  Matukiodaimablog
Kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited imewapongeza wateja  wake kwa  kuendelea  kutoa ushirikiano kwa  kutumia bidhaa  zake .

  Afisa masoko wa kampuni ya maziwa ya Asas  Dairies Ltd ya mkoani Iringa Bw Jimy Kiwelu alisema  hayo  leo  wakati akitoa  salam  za mwaka mpya 2015 na  kutambulisha mwonekano mpya  wa  kisasa  zaidi wa chupa  za maziwa  ya kampuni   hiyo kwa  sasa.

Alisema  mbali  ya mafanikio makubwa  ambayo kampuni  hiyo  imefanikiwa  kuyafikia kwa kuendelea kupata tuzo ya  ubora  wa  maziwa  kwa  miaka takribani  miwili  sasa  bado  kampuni  hiyo  imejipanga kuporomoka katika ubora  na katika  kuhakikisha wanaendelea  kushikilia nafasi ya  kwanza na ubora wa maziwa nchini Tanzania   hivi  sasa tayari kampuni hiyo  imekuja na mwonekano mpya  wa maziwa  yake kwa kuwa  katika  chupa tofauti  na zile  za mwanzo .
Furaha ya  bidhaa mpya ya  asas Dairies Ltd  katika  mwonekano  mpya

Hata hivyo  alisema  kuwa  kuanzisha mwonekano  mpya  wa chupa  za maziwa  hayo  kumekwenda   sambamba na  kuongeza  ubora  zaidi  wa  bidhaa  hizo  hivyo kuwakata watumiaji wa bidhaa  zao  kuanza  kufurahia  kuaga mwaka 2014 na  kuukaribisha  mwaka 2015 kwa  kutumia maziwa yenye  mwonekano tofauti na  ule  wa  mwanzo .
                                     Mwonekano  wa  zamani 
Pia alisema kampuni  yake  imekuwa  mbele  katika  kuchangia maendeleo  ya mkoa  wa Iringa kama sehemu ya kutambua ushirikiano mkubwa  wa kampuni kwa maendeleo ya Taifa .

Kiwelu alitaja moja kati ya  shughuli ambazo kampuni imepata  kusaidia kuwa ni pamoja na kuhamasisha  jamii ya  Iringa  na  watanzania  kupenda  kunywa maziwa  kwa afya badala ya  kutumia muda  wao  kuingiza  sumu mwilini kwa kunywa  pombe pia kampuni imepata kutoa  msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.7 kwa shule za msingi tatu ambazo zilishinda katika mashindano ya uchoraji wa picha zinazoelezea umuhimu wa unywaji maziwa mashuleni

Mbali ya zawadi hizo kwa shule hizo tatu pia kampuni hiyo ilipata kuwanywesha maziwa wanafunzi zaidi ya 30,000 wa shule za msingi katika Manispaa ya Iringa.

Shule hizo zilizopatiwa msaada wa madawati ni pamoja na Hoho iliyoshika nafasi ya kwanza na kupata madawati yenye thamani ya Tsh milioni 1 ,Mlangali iliyoshika nafasi ya pili na kupata madawati ya Tsh.750,000 pamoja na St Dominic iliyopata madawati yenye thamani ya Tsh 500,000.

Saturday 22 November 2014

KAMPUNI YA CONTINENTAL RELIABL CLEANRING (T) LTD YAJIVUNIA KWA UAMINIFU WA ULIPAJI KODI NCHINI

Hiki  ndicho  cheti  cha ushindi ambacho kampuni ya Continental Reliable Cleanring (T)  Ltd  inayounda  pia kampuni  za  Fm Abri na Famari Inverstment (T) Ltd
Wawakilishi  wa kampuni ya Continental Reliable Cleanring (T)  Ltd and Fm Abri /Famari Inverstment (T) Ltd wakiwa katika maadhimisho hayo ya TRA mkoa  wa Dar es Salaam jana
Mwakilishi  wa Continental Reliable Cleanring (T)  Ltd and Fm Abri Bw  Fahad Abri  akiwa katika ukumbi  huo
Continental Reliable Cleanring (T)  Ltd  wakiwa katika ukumbi huo

KAMPUNI ya kizalendo ya  Continental Reliable Cleanring (T)   Ltd iliyopo  chini ya kamapuni ya  Fm Abri na Famari Inverstment (T) Ltd  yenye makao  yake mjini Iringa na Dar es  Salaam  imejipongeza  kwa  kufanikiwa  kuongoza nafasi ya  tatu katika mkoa  wa Dar e Salaam  kwa  ulipaji mzuri  wa  kodi nchini.

Akizungumza  mara  baada ya  kukabidhiwa   cheti hicho jana katika  maadhimisho ya  siku ya mlipa  kodi yaliyofanyika kitaifa  katika Ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam  mkurugenzi mtendaji  wa kampuni hiyo Bw Abbdalallah Abri  alisema  kuwa kampuni  yake  inajivunia kwa  kushika  nafasi ya  tatu kwa mkoa  wa Dar es Salaam  kwa  ulipaji mzuri wa  kodi.

Hapa  hivyo  alisema mafanikio hayo  yanaiwezesha kampuni  hiyo  kuendelea  kujenga  heshima  kubwa katika Taifa ila  pia  kuongeza  ufanisi  zaidi  wa utendaji kazi  wake na hali ya uaminifu ambayo  ndio msingi mkubwa kwa maendeleo ya Taifa .

Abri  alisema  kuwa  ili  Taifa   kuendelea  kujenga uchimi imara   ni  wajibu  wa kila mfanyabiashara   kuonyesha  uzalendo wake  kwa  kulipa  kodi na kuwa   wao kama wamiliki  wa kampuni ya  kizalendo ya Continental Reliable Cleanring (T)  Ltd iliyopo chini ya kamapuni ya  Fm Abri  na Famari Inverstment (T) Ltd kamwe  hawatakuwa  nyuma katika ulipaji  kodi  nchini.

" Kweli  tunajivunia nafasi hii ambayo tumeishika kuwa nafasi ya tatu kwa  mkoa kama Dar es Salaam ambao  una makampuni  mengi zaidi na  wafanyabiashara wengi  wakubwa ni jambo la  kujivunia sana "

Hata  hivyo  alisema  kuwa  ushindi  ambao kampuni hiyo  imeupata  wa  ulipaji kodi  ni heshima  pia  kwa  wateja  wake ambao  wameendelea  kujenga imani na kampuni  hiyo kwa kuendelea  kuitumia katika uagizaji  mizigo mbali mbali yakiwemo magari na  kuwa heshima hiyo itaendelea  kujengwa  zaidi na makampuni   yote yaliyopo chini ya Continental Reliable Cleanring (T)  Ltd  na mengine  yanayomilikiwa na Fm Abri .

Friday 21 November 2014

KAMPUNI ZA ASAS ZAONGOZA KWA ULIPAJI KODI BORA KWA MKOA WA IRINGA

Mlipaji kodi mdogo mkoa wa Iringa  Shakra  kiwanga akionyesha  cheti alichokabidhiwa  na TRA leo
Mkurugenzi  wa makampuni ya  Asas  Bw  Salim Abri  Asas  kushoto akipokea cheti  maalum kutoka kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Letici Warioba  baada ya  kuibuka  mshindi wa kwanza katika  ulipaji kodi mkoa wa Iringa leo
Meneja  wa TRA mkoa wa Iringa Rosalia Mwenda akimpongeza  Bw  Asas  kwa ushindi katika ulipaji kodi
Cheti  kilichotolewa kwa  kampuni ya Asas
Salim Asas  akionyesha  cheti kwa wanahabari  baada ya  kukabidhiwa  cheti  hicho kwa kuwa mlipaji  kodi mzuri
Salim Asas akionyesha  cheti  cha ulipaji kodi bora 
Mzee Kaundama  akipokea  cheti
Meneja  wa TRA  Iringa Bi Mwenda akitoa maelezo ya  awali
Meza  kuu
Mfanyabiashara  Kaundama akijitambulisha
Wanafunzi  wakiigiza  igizo la matumizi ya mashine ya EFDS
Wadau wa TRA  Iringa  wakiwa katika sherehe ya siku ya mlipa kodi
Baadhi ya  waalikwa wakishuhudia
Msanii Iringa akionyesha ujuzi wa kucheza na nyoka aina ya chatu
Wanafunzi wakihamasisha  ulipaji kodi
Watumishi wa TRA  Iringa  wakijadili jambo kabla ya  sherehe hiyo kuanza
Mgeni  rasmi katika  siku ya mlipa kodi mkoa wa Iringa Dr  Leticia  warioba kulia akimkabidhi cheti  mfanyabiashara  Salim Asas   kutoka makampuni ya usafirishaji  mizigo   la Asas Transporters Co. Ltd    na  ile ya   usafilishaji wa mafuta ya  TransFuel Logistics Ltd  baada ya  kuongoza  kwa  ulipaji mzuri  wa  kodi kwa mwaka 2013 /2014
Mgeni  rasmi katika  siku ya mlipa kodi mkoa wa Iringa Dr  Leticia  warioba kulia akimkabidhi cheti  mfanyabiashara  Salim Asas   kutoka makampuni ya usafirishaji  mizigo   la Asas Transporters Co. Ltd    na  ile ya   usafilishaji wa mafuta ya  TransFuel Logistics Ltd  baada ya  kuongoza  kwa  ulipaji mzuri  wa  kodi kwa mwaka 2013 /2014.
Mlipaji kodi mdogo Iringa Shakra  kiwanga akippongezwa kwa  ushindi wa  pili
Salim Asas  akihojiwa na  wanahabari  mkoani Iringa kuhusu  tuzo  mbili alkizopata kwa kuongoza katika ulipaji wa kodi mkoa wa Iringa
Waandishi  wa habari Iringa  wakimhoji Salim Asas  baada ya  kutangazwa mshindi wa kwanza kwa  ulipaji mzuri wa kodi mkoa wa Iringa
Na matukiodaimaBlogu.
WAKATI maadhimisho ya  siku ya mlipakodi nchini yameadhimisha leo nchini kote mamlaka ya mapato  Tanzania (TRA) mkoa  wa Iringa  imekabidhi  tuzo  mbili kwa a makampuni mawili  yanayomilikiwa na familia ya kamanda wa UV CCM mkoa  wa Iringa Bw Salim Asas likiwemo kampuni la  usafirishaji  mizigo   la Asas Transporters Co. Ltd    na  ile ya   usafilishaji wa mafuta ya  TransFuel Logistics Ltd  baada ya  kuongoza  kwa  ulipaji mzuri  wa  kodi kwa mwaka 2013 /2014.


Akitangaza  washindi hao   wakati  wa maadhimisho ya  siku ya mlipa kodi yaliyofanyika  kimkoa katika ukumbi wa IDYDC  mjini Iringa meneja  wa  mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa  wa Iringa Rosalia Mwenda alisema  kuwa    TRA  imekuwa na utaratibu  wa  kuadhimisha  siku ya mlipa kodi nchini na kuwa kwa  mkoa wa Iringa na  Njombe maadhimisho hayo yamefanyika katika mkoa  wa Iringa  kutokana na mamlaka  hiyo  kuendelea kufanya kazi kama mkoa mmoja .

Alisema  kuwa kampuni  hizo  za  Asas  zimeweza  kuongoza katika  ulipaji kodi katika kipengele  cha mfanyabiashara mlipaji kodi mkubwa baada ya  makampuni mawili  yanayosimamiwa na Asas moja kushika nafasi ya kwanza ambalo ni  lile  kampuni ya  usafirishaji ya Asas Transporters  C. Ltd    kwa  ulipaji kodi  na nafasi ya  pili ya walipaji kodi wa kati  pia imechukuliwa na  kampuni ya usafirishaji  mafuta ya Transfuel Logistics Ltd ambayo  pia  ni  sehemu ya makampuni ya shiriki ya Asas

Aliwataja  wengine   walioongoza katika  ulipaji kodi  kuwa ni pamoja na MT Huel Transporters , ambayo  ilishika nafasi ya  pili na nafasi ya tatu  kwa  walipaji  kodi wakubwa ni  pamoja na Ruaha  University  College   huku  upande  wa  walipaji  kodi  wa kati  aliyeongoza na Iringa Foods and  Deverages Ltd  nafasi ya  pili Transfuel Logistics Ltd na nafasi ya tatu  Kalenga West Parki Tours MOtel Ltd .

Wakati kwa  wafanyabiashara  wadogo  walioshinda  tuzo  hizo  za  vyeti  maalum  nafasi ya  ya kwanza  alipewa BEder F. Kileo nafasi ya  pili  ilichukuliwa na Shakra  Kiwanga  ambae ni mwenyekiti  wa UWT  wilaya ya  Iringa na nafasi ya  tatu  ilichukuliwa na Ahmed Tasha wakati  kwa  mshindi  wa  jumla  kwa mkoa wa Iringa na kanda ya nyanda  za  juu  kusini akipewa  tuzo hiyo Sao Hill Forest Project .

Kwa  upande  wa  vituo vya  radio   kampuni ya  Big  Time  Hinghland  co.Ltd(Radio  Ebony Fm) nafasi ya  pili kampuni ya  Scope Tanzania Ltd ( Radio Countyr  Fm) na nafasi  ya  tatu Qiblatain  Fm  Radio .

Wakati  kwa upande  wa  walipakodi  bora  wilayani  kwa    Mufindi ni SAo Hill Forest Project  iliyoshika nafasi ya  kwanza na ya pili na ya tatu  kuchukuliwa na Chai Bora Ltd  wakati  wilaya ya Ludewa  ni John  Naoel Haule   ,nafasi ya pili  ni Donata Linus MGaya  huku nafasi ya tatu   ni Nathanael Mgaya ,  katika  wilaya ya  Makete  aliyeongoza ni Felix Eliud Sanga , Christopher s.   Mahenge  na  nafasi ya Tatu ni Shaibustolen  Mahenge .

Wilaya ya  Njombe  mshindi  wa kwanza ni  Philemon N . Mtewele   nafasi ya  pili ni Augustino L . Kisinga  na nafasi ya tatu kwa  ulipaji kodi ni  Ndimi Enterprises Ltd .

Akizungumza  baada ya  kukabidhiwa   tuzo  hiyo  mkurugenzi  wa kampuni  za  Asas  Bw  Salim Abri asas  ambae ni kamanda wa UV CCM mkoa  wa Iringa  alisem a kuwa  wajibu  wa kampuni yake ni  kuendelea  kulipa kodi vizuri kama  sehemu ya  kukuza uchumi wa Taifa na  kuwa  tuzo hizo ni  heshima kwa kampuni  zake na kuwa  ni chachu kwa  wengine  kupenda  kulipa kodi .

Pia  alisema  wapo ambao wanafikra  tofauti  kuwa  ukiwa mwanasiasa  ni mtu  wa  kukwepa  kodi na  kuwa kampuni  zake  zipo kwa ajili ya  kuona  uchumi wa Taifa  unakua  pamoja na kulipa  kodi kwa  wakati na  kwa mujibu  wa taratibu za  nchi .

Hata  hivyo  alisema kuwa ukwepaji  kodi  hausaidii hata  kidogo kwa ukuzaji wa uchumi wa Taifa na  kuwa kila mfanyabiashara  anapaswa  kuwa mzalendo na Taifa  lake kwa  kulipa  kodi badala ya  kukwepa  kulipa  kodi .

" Na mimi napenda  kushukuru  sana TRA kwa utaratibu  huu wa  kuwatambua walipaji kodi wazuri na kuwapa vyeti hii ni heshima  na changamoto  kubwa kwa wafanyabiashara  wengine  kulipa  kodi vizuri "

Tuesday 29 July 2014

IDDI YAMALIZIKA KWA MAJANGA IRINGA MMOJA AFARIKI DUNIA UWANJANI


  Halida Ng'anguli akiwa ameanguka  nje ya  choo  katika  uwanja  wa Samora kabla ya  kufariki dunia (picha na  kikosi kazi cha matukiodaimaBlog)
kaimu sheikh wa  mkoa  wa  Iringa  Abubakar Chalamila
..................................................................................................................................................
WAKATI  waislamu   nchini  jana  wameungana na  waislamu  wenzao duniani kuswali  sala  ya Iddi mkoani  Iringa swali   hiyo  imemalizika  vibaya  kufuatia kifo  cha  muumini  mwenzao Halida Ng'anguli mkai  wa Mwangata  C ambae ni shangazi wa manahabari wa gazeti la majira  Iringa Zuhura  zuhkeri kufariki  dunia  baada ya masaa machache  toka aanguke chooni uwanja wa  Samora.



Tukio  la  kuanguka kwa mwanamke   huyo  lilitokea majira ya  saa tatu  asubuhi wakati  waumini  wa dini ya  Kiislamu  ambao  walikuwa  wakiswali pamoja  katika  uwanja  wa samora mjini Iringa  kumaliza swala na  kuanza maandalizi ya kuondoka  uwanjani  hapo kabla ya mmoja kati ya  viongozi  kwa kutumia kipasa  sauti  kutangaza  tukio la  kuanguka kwa mwanamke  huyo huku akiwataka  wanawake kwenda  eneo la tukio katika  vyoo vya wanawake  ili  kutoa msaada  zaidi.

Hata  hivyo  jitihada za  waumini  hao wanawake  pamoja na  askari  waliokuwepo  uwanjani hapo  zilifanikisha  kumkimbiza  mweanamke  huyo  hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.

Ibada ya  idd ikiendelea katika uwanja wa Samora mjini Iringa   
 ............................................................................................
Mbali ya  jitihada  kubwa  za madaktari wa Hospitali  hiyo  kutaka kunusuru maisha  yake  bado  hali ilionekana  kuwa mbaya  zaidi kutoka na tatizo ya  ugonjwa wa kisukari lililokuwa  likimsumbua .

Yapata  majira ya saa 4  usiku mwanamke  huyo alifariki dunia  wakati  akiendelea  kupatiwa matibabu  Hospitalini  hapo.
  Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza wa tatu  kushoto akishiriki ibada ya Iddi

 Mwanahabari  Zuhura Zukheri wa tatu kushoto akiwa na mwanahabari Clement Sanga kulia  na mmiliki wa mtandao huu mzee wa matukiodaima wakipata nyama wakati wa  ziara ya kuelekea mikoa ya kaskazini kutangaza utalii wa ndani .
.....................................................................................
Akithibitisha   kutokea  kwa  kifo  hicho Shangazi wa marehemu  mwanahabari  Zuhura Zukheri alisema  kuwa shangazi yake  alifariki  majira ya saa 4 akiwa katika matibabu na  kuwa  toka  alipofikishwa  Hospitali hapo  hari yake  ilikuwa  mbaya na  hakuweza kupata nafuu.

Zuhura  alisema  kuwa tatizo kubwa  lililokuwa likimsumbua ni ugonjwa wa  Kisukari  na  kuwa shughuli za mazishi  zimepangwa  kufanyika  leo  ambayo ni  siku ya  Iddi pili majira ya saa 10 jionini .

Uongozi  wa chama  cha waandishi wa habari  mkoa  wa Iringa (IPC) unaungana na familia ya  mwanahabari huyo  Zuhura  Zukheri katika  wakati  huu mgumu  wa maombolezo ya  kifo cha mpendwa  wetu  huyo ,

Wednesday 9 July 2014

DIWANI WA TLP LUPINGU ASEMA YEYE SI MPINZANI ,AMFAGILIA MBUNGE FILIKUNJOMBE KWA KASI YA MAENDELEO

Diwani wa kata ya Lupingu  wilaya ya  Ludewa  John Kiowi kulia  akiwa amevalia sare za CCM huku akieleza imani yake  kwa mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe katika  kuwatumikia  wananchi wa jimbo la Ludewa na kudai kuwa  yeye  si mpinzani kama wengine ,  kushoto ni mbunge  Filikunjombe akimsikiliza kwa makini  wakati wa shughuli  ya maendeleo ya kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kwenda Lupingu
Mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo  Filikunjombe kushoto akishiriki  kubeba  nguzo za umeme  wakati wa uhimizaji wa wananchi wa kata ya Lupingu kushiriki maendeleo ya  kupeleka  umeme kata ya Lupingu 
Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akishiriki  kubeba  nguzo
Vijana  wakishirikiana na mbunge  wao kubeba nguzo za umeme
jitihada za kupeleka  umeme  Lupingu  zikionekana
Mbunge wa jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe akiwa  chini ya shimo akiendelea  kuchimba shimo kwa ajili ya nguzo ya umeme kwenda  kata ya Lupingu kutoka Ludewa ,kushoto ni  diwani wa TLP kata ya Lupingu John Kiowi akishirikiana na mbunge huyo
Mbunge  Filikunjombe shimoni na diwani wa TLP  wakishiriki kuchimba mashimo ya nguzo za umeme
Mbunge  wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe akishiriki  kuchimba mashimo ya  nguzo za umeme pamoja na wananchi wa kata ya Lupingu

DIWANI  wa  chama   cha Tanzania Labour Party (TLP) kata ya  Lupingu  wilaya ya  Ludewa mkoani  Njombe  John Kiowi amempongeza  mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kwa jitihada zake   anazozifanya katika  kuwapelekea maendeleo wananchi wa Ludewa  huku akiwashangaa   wapinzani wanaopinga  jitihada  mbali mbali  zinazofanywa na serikali ya  chama  cha Mapinduzi (CCM) na  kudai  kuwa  yeye  si mpinzani wa uchwara wa  kupinga  maendeleo .

Akizungumza   na  wanahabari  jana wakati wa  zoezi la mbunge  Filikunjombe  na  diwani  huyo  kushiriki na  wananchi  wa kata ya  Lupingu  kuchimba mashimo ya nguzo  za umeme  na kusimika  nguzo hizo za umeme , Kiowi  alisema  kuwa   ni  zaidi ya  wabunge  watano  wamepata  kuliongoza  jimbo  hilo la Ludewa  ila ni mara  yake ya kwanza  kuona mbunge akishiriki bega kwa  bega na wananchi wake  kuchimba mashimo  kama ambavyo mbunge  huyo anafanya .

" Jamani  wananchi  kwanza ni jambo la kumpongeza mbunge  wetu mbali ya kuhimiza wananchi ila mwenyewe  pia amekuwa mstali wa mbele katika  kushiriki tofauti na wana siasa  wengine ambao  muda  wote  wao ni watu wa majukwaani ila  vitendo sifuri .....nasema  Ludewa  imempata mbunge na niweke  wazi  hapa mimi  sio mpinzani hivi  tujiulize wenyewe  nikisema mimi ni mpinzani napinga  nini hapa haya maendeleo  ni kwa  faida yangu na  wananchi  wote  sasa kama mbunge wa CCM wanafanya  kuna haja ya upinzani hapa "

Kiowi  alisema kuwa ataendelea  kufanya kazi na mbunge  Filikunjombe ikiwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata  yake kwani chama  chake  cha TLP katika  kata ya Lupingu  kinatekeleza  ilani ya  CCM ambacho  ndicho  chama  kilichopo madarakani na peke  yake  bila kumtegemea  mbunge hawezi  kufanya lolote.

Diwani Kiowi ambae  alikuwa amevalia  sare  za CCM katika  shughuli  hiyo ya maendeleo  alisema kuwa  katika kuhakikisha kuwa yeye  si mpinzani ila ni mpenda maendeleo  hata  sare za CCM zinazotolewa na mbunge Filikunjombe amekuwa akizivaa na amekuwa mstali wa  mbele kumpongeza  mbunge  huyo kutokana na kuwa mbunge wa mfano kwa kufanya kazi bila na makundi  yote .

Hata   hivyo  diwani  huyo alisema kuwa katika  suala la maendeleo hata  kuwa tayari kuona  watu  wachache  wakimkwamisha mbunge  huyo kwa  kushindwa kuunga mkono jitihada  zake katika kuwaletea maendeleo na kudai kuwa  kwa  upande  wake anaona  wapinzani ni  wana CCM wenyewe wasiopenda kujivunia maendeleo makubwa mbayo  mbunge  Filikunjombe ameyapeleka Ludewa .

Kwa  upande wake  mbunge  Filikunjombe mbali ya kumpongeza diwani  huyo wa TLP kwa  kushiriki  vema katika  shughuli za maendeleo bado  alisema kuwa ni  wapinzani wachache nchini ambao  wanajitoa kama  diwani  huyo katika  shughuli za maendeleo  zinazoitishwa na mbunge wa CCM

Alisema yapo  baadhi ya maeneo  wabunge ama madiwani wa upinzani  wamekuwa ni watu wa  kupinga kila jambo linalofanywa na mbunge ama diwani wa CCM  na  wengine  wasiokuwa na uzalendo  na Taifa  wamefikia hatua ya kubeza hata jitihada zinazofanywa na Rais Dr Jakaya  Kikwete katika  kuliletea maendeleo  Taifa  jambo ambalo si la kizalendo hata kidogo na kuwa  huo si upinzani wa kweli.

" Nataka  kusema  hivi wakati  wa kampeni ndio  wakati wa kupingana kisera ila baada ya chaguzi  hakuna  haja ya  kuendelea  kupingana ni kuwa  wamoja na kuwaletea  wananchi maendeleo hivi  hebu  niulize ujenzi huu wa barabara  ya Lupingu ,Ludewa  na Njombe Ludewa unaoendelea ni kwa  faida ya nani hii barabara  inatumiwa na wana CCM pekee  mbona  hata  wapinzani mnapita katika barabara  hiyo  hiyo  sasa unapinga  nini wakati  huu wa CCM kutekeleza ilani  yake ....tuwe  na uzalendo  wa nchi  yetu tusiwe wa  kupinga kila  kitu na mimi nikueleze  wazi kama  ungejaribu kupinga mradi huu wa umeme  kwa  kutoshiriki tungeonana  wabaya mbele ya  safari"

Akielezea  mradi huo wa umeme Filikunjombe  alisema kuwa kwa kasi  ambayo  wananchi  wanaenda nayo katika  kujitolea  nguvu  zao kuchimba mashimo na  kusogeza nguzo katika mashimo  hayo ni  wazi  mradi huo wa umeme  utakamilika kabla ya  Desemba mwaka  huu .

Aidha  alisema kuwa wakati akiingia madarakani mwaka 2010  ni  kijiji  kimoja pekee cha jimbo  hilo la Ludewa ambacho  kilikuwa na umeme  wa mafuta  ila  sasa  zaidi  ya vijiji 10  vina umeme na kuwa hadi sasa   jumla ya  vijiji 49 vitafikiwa na mradi wa umeme huo ambao unatekelezwa kwa nguvu za  serikali ya Tanzania , Swedeni na kanisa na Romani Katoliki Dayosisi ya  Njombe.