Friday 6 June 2014

WANANCHI KATA YA NZIHI JIMBO LA KALENGA WAMPONGEZA MBUNGE MGIMWA WASEMA NI MBUNGE HAWATAKI MWINGINE, MWENYEWE AWATAKA KUTOA USHIRIKIANO ZAIDI


Wazee kijiji cha Nyamihuu wakimpa baraka na kumpongeza mbunge  Mgimwa  kwa uchapa kazi wake 
MBUNGE  wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa amesema atahakikisha anafanya kazi na  vyama  vyote vya  siasa na  kuwa kuwataka  wananchi wa  jimbo la Kalenga kuachana na makundi  ya vyama vya siasa na kuunagana  pamoja  ili  kufanikisha  jimbo hilo kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

Mbali ya  kuwataka kuachana na makundi  ya kisiasa  pia amewataka  waliokuwa  wagombea  wa nafasi za ubunge katika uchaguzi mdogo  kupitia  CCM kuacha  kujipitisha  kwa  sasa kwa  wananchi na badala yake kusubiri uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Akizungumza kwa nyakati  tofauti katika  mikutano yake ya hadhara  kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa  kumchagua na leo katika kata ya Nzihi ,mbunge huyo  alisema kuwa amelazimika  kuomba ruhusa bungeni kwa  spika  ili kurudi  kuwashukuru  wananchi hao hasa  kutokana na upendo mkubwa ambao  wananchi wa jimbo hilo  walionyesha kwake.

"Ndugu  zangu nilianza  kuzunguka katika baadhi ya maeneo  na kutekeleza ahadi  mbali mbali hata kabla ya  kuapishwa  rasmi  bungeni ......na nitajitahidi kulingana na uwezo wangu  ili kuona natimiza wajibu  wangu kwenu na kamwe  sitawaangusha ndani ya bunge na nje ya  bunge"

Hivyo  aliwataka  wananchi  kwa umoja  wao kuendelea  kumuombea afya  njema  ili kufanikisha  kutimiza ndoto  yake ya  kufikisha maendeleo  katika  jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kutimiza sehemu kubwa ya ahadi ambazo zilitolewa na marehemu Dr Wiliam Mgimwa aliyekuwa  mbunge  wa  jimbo  hilo.

Kuhusu  suala la kuyawezesha makundi mbali mbali Mbunge Mgimwa  aliwataka  wananchi  kujiunga na vikundi  vya VICOBA ili  kuviwezesha  vikundi  hivyo  kiuchumi zaidi badala ya  kuwa mtu mmoja mmoja na kuwataka  wazee  pia  kuanzisha umoja  wao na  kupeleka mahitaji yao katika  ofisi  yake.

"Kuna  vikundi  vya VICOBA ambavyo tayari  vimeanzishwa na   moja kati ya  vikundi  hivyo  tayari  nimechangia kiasi  cha Tsh 500,000 na nitaendelea  kuchangia na kuna eneo ambalo marehemu mbunge wetu aliyepita aliahidi kuchangia milioni 1 katika  kikundi cha VICOBA Magubike nasema  fedha  hizo  nitazitoa  mimi "

Alisema  kuwa tayari ameanza  kupigania  suala la umeme na maji katika  vijiji  vya jimbo la Kalenga  bungeni na kuwa  mawaziri wa  wizara  hizo  wameahidi  kulifanyia kazi na kuendelea kusaidia miradi hiyo mikubwa ambazo ndizo ahadi  kubwa  zaidi.

Awali  wananchi  wa kijiji cha Magubike  walimpongeza mbunge  huyo na  kuwa katika historia ya  jimbo la Kalenga  hawajapata kuwa na mbunge mkweli na mchakakazi kama  huyo na kurudi mapema zaidi kwa wananchi kuwashukuru na hivyo kumhakikishia  kuwa hawana mpango wa kumchagua mbunge mwingine mwaka 2015 na kukiomba chama cha mapinduzi kumbariki kuendelea  kuongoza jimbo hilo .

Kwa  upande  wake katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Iringa Denis Lupala alisema  kuwa utendaji kazi mzuri wa mbunge  huo ndio ambao unakishawishi  chama kuendelea  kumpa ushirikiano zaidi na kuwa wananchi hawana sababu ya kubabaishwa na wapinzani ambao  wameanza kujipitisha katika  jimbo hilo.

MBUNGE MGIMWA AANZA KUTIMIZA AHADI ZA MAREHEMU BABAKE KWA KASI KUBWA


'Hongera  sana mheshimiwa kweli umeanza kwa mfano "
Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Iringa Denis Lupala kulia akimpongeza diwani wa kata ya Nzihi kwa kazi nzuri 
Wananchi wa Ilala  Simba  wakimsikiliza mbunge Mgimwa 
Uongozi wa kijiji cha Ilala Simba  ukimkabidhi mbunge Mgimwa risala yao 
Mbunge Mgimwa akikabidhi mipira  kijiji cha Ilala  Simba leo 
Sehemu ya  saruji  iliyotolewa  leo na mbunge Mgimwa 
Mbunge  wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Nyamihuu katika  ziara  yake ya  kuwashukuru na kupokea  changamoto mbali mbali 
Mmoja kati ya  wazee  walemavu kijiji  cha Nyamihuu kalenga  akimwomba mbunge Mgimwa msaada wa baiskeli ya  walemavu 
Kiongozi wa  serikali ya  kijiji cha Nyamihuu akipokea mipira kwa ajili ya kuendeleza michezo kwa  vijana
Wazee kijiji cha Nyamihuu wakimpa baraka na kumpongeza mbunge  Mgimwa  kwa uchapa kazi wake 
Bw  Kiswaga  akimpongeza mbunge Mgimwa kwa kuonyesha usikivu mkubwa kwa wananchi 
Wananchi wa kijiji cha Nyamihuu wakimshangilia mbunge Mgimwa  leo 
Wananchi wa Kidamali  wakimsalimia mbunge Mgimwa leo  huku  wakifurahia utendaji kazi wake 
Mbunge Mgimwa akifurahi na  watoto wa kijiji cha Kidamali  waliofika  kumsalimia 
Mbunge Mgimwa akisalimiana na  wananchi pamoja na watoto  waliomng'ang'ania leo amini ni mbunge  wa  wote 
Diwani wa kata ya Nzihi Stivin Mhapa akimpongeza mbunge Mgimwa  leo 
Wananchi wa Kidamali  wakimsikiliza mbunge Mgimwa kwa umakini mkubwa 
Katibu mwenezi wa CCM Iringa Danis Lupala akimkaribisha mbunge Mgimwa  leo 
Mbunge Mgimwa akiwashukuru  wakazi wa Kidamali 
Mbunge Mgimwa  kulia akikabidhi mipira kwa vijana leo 
Mbunge Mgimwa  kulia akikabidhi msaada wa  saruji mifuko 50 kwa ajili ya kuchangia ujenzi kijiji cha Kidamali leo 
Mbunge Msigwa akikabidhi fedha  taslimu kiasi cha Tsh 500,000 kuchangia  michezo na ujenzi wa  soko 
Mbunge Mgimwa akisalimiana na  wananchi wa kidamali  leo 

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Magubike Bi Lenatha Mbilinyi kushoto akipokea msaada wa saruji mifuko 100 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa leo ,wanaoshuhudia  kulia ni katibu menezi wa CCM wilaya Denis Lupala na diwani wa kata ya Nzihi katikati Bw Stivin Mhapa
........................................................................................

MBUNGE  wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa  Godfrey Mgimwa ameanza  kutimiza ahadi  zake kwa  wananchi  wa  jimbo la kalenga  kwa  kukabidhi mifuko zaidi ya 150 ya  saruji katika  kijiji cha Magubike na kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi  yenye  thamani  ya zaidi ya Tsh milioni 2.5


Saruji  hiyo mifuko 100 kwa ajili ya  kusaidia ujenzi wa jengo la utawala shule ya  sekondari Dimitrios katika  kijiji  cha Magubike  na mifuko 50 kwa ajili ya shule ya sekondari Kidamali.


Mgimwa alisema kuwa lengo la kutimiza ahadi  yake  hiyo ni kama njia ya  kuwashukuru  wana Kalenga kwa kumchagua katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni pia kutimiza ahadi mbali mbali binafsi ambazo alizitoa mbunge aliyefariki marehemu Dr Wiliam Mgimwa.


Alisema ataendelea  kutimiza ahadi  binafsi zilizotolewa na marehemu Dr Mgimwa kulingana na uwezo  wake  na zile  za  kitaifa ambazo zipo katika Ilani ya CCM atahakikisha anaikumbusha  serikali  ya CCM ili  kutimiza ahadi hizo kwa  wakati.

“Ndugu  zangu wananchi  mbali  ya  kuwa  ubunge  wangu ni  wa  mwaka mmoja  ila  tayari  mimeanza  kutimiza ahadi  bila  ya kuchelewa  na  ninawahakikishieni  sita  waangusha  nitaendelea  kufanya  hivyo  zaidi  mniombee  uzima”


Alitaja  maeneo  ambayo tayari  amekabidhi  ahadi  zilizotolewa na mbunge aliyefariki  kuwa ni pamoja  na Kiwere shule ya msingi mifuko 80 ya saruji,shule  ya msingi wangama bati 100 na  saruji mifuko 50,shule ya msingi Negabii bati 100 ,shule ya msingi Mibikimitali bati 50 ,Kijiji cha Isupilo bati  50 na saruji mifuko 50 na maeneo mingine mengi.


Pia amekabidhi kiasi cha  Tsh 500,000 kwa ajili ya kuchangia kuwezesha  kusajili  timu ya  kata ya Nzihi na nyingine  kwa ajili ya ukarabati wa soko