DIWANI wa chama cha Tanzania
Labour Party (TLP) kata ya Lupingu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe
John Kiowi amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa
jitihada zake anazozifanya katika
kuwapelekea maendeleo wananchi wa Ludewa huku akiwashangaa wapinzani
wanaopinga jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali ya chama
cha Mapinduzi (CCM) na kudai kuwa yeye si mpinzani wa uchwara wa
kupinga maendeleo .
Akizungumza
na wanahabari jana wakati wa zoezi la mbunge Filikunjombe na
diwani huyo kushiriki na wananchi wa kata ya
Lupingu kuchimba mashimo ya nguzo za umeme na kusimika nguzo hizo
za umeme , Kiowi alisema kuwa ni zaidi ya wabunge watano
wamepata kuliongoza jimbo hilo la Ludewa ila ni mara yake ya
kwanza kuona mbunge akishiriki bega kwa bega na wananchi wake
kuchimba mashimo kama ambavyo mbunge huyo anafanya .
"
Jamani wananchi kwanza ni jambo la kumpongeza
mbunge wetu mbali ya kuhimiza wananchi ila mwenyewe pia amekuwa
mstali wa mbele katika kushiriki tofauti na wana siasa wengine ambao
muda wote wao ni watu wa majukwaani ila vitendo sifuri .....nasema
Ludewa imempata mbunge na niweke wazi hapa mimi sio mpinzani hivi
tujiulize wenyewe nikisema mimi ni mpinzani napinga nini hapa haya
maendeleo ni kwa faida yangu na wananchi wote sasa kama mbunge wa
CCM wanafanya kuna haja ya upinzani hapa "
Kiowi
alisema kuwa ataendelea kufanya kazi na mbunge Filikunjombe ikiwa ni
pamoja na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata yake kwani
chama chake cha TLP katika kata ya Lupingu kinatekeleza ilani ya
CCM ambacho ndicho chama kilichopo madarakani na peke yake bila
kumtegemea mbunge hawezi kufanya lolote.
Diwani
Kiowi ambae alikuwa amevalia sare za CCM katika shughuli hiyo ya
maendeleo alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa yeye si mpinzani ila
ni mpenda maendeleo hata sare za CCM zinazotolewa na mbunge
Filikunjombe amekuwa akizivaa na amekuwa mstali wa mbele kumpongeza
mbunge huyo kutokana na kuwa mbunge wa mfano kwa kufanya kazi bila na
makundi yote .
Hata
hivyo diwani huyo alisema kuwa katika suala la maendeleo hata kuwa
tayari
kuona watu wachache wakimkwamisha mbunge huyo kwa kushindwa kuunga
mkono jitihada zake katika kuwaletea maendeleo na kudai kuwa kwa
upande wake anaona wapinzani ni wana CCM wenyewe wasiopenda kujivunia
maendeleo makubwa mbayo mbunge Filikunjombe ameyapeleka Ludewa .
Kwa
upande wake mbunge Filikunjombe mbali ya kumpongeza diwani huyo wa
TLP kwa kushiriki vema katika shughuli za maendeleo bado alisema
kuwa ni wapinzani wachache
nchini ambao wanajitoa kama diwani huyo katika shughuli za
maendeleo zinazoitishwa na mbunge wa CCM
Alisema
yapo baadhi ya maeneo wabunge ama madiwani wa upinzani wamekuwa ni
watu wa kupinga kila jambo linalofanywa na mbunge ama diwani wa CCM
na wengine wasiokuwa na uzalendo na Taifa wamefikia hatua ya kubeza
hata jitihada zinazofanywa na Rais Dr Jakaya Kikwete katika kuliletea
maendeleo Taifa jambo ambalo si la kizalendo hata kidogo na
kuwa huo si upinzani wa kweli.
"
Nataka kusema hivi wakati wa kampeni ndio wakati wa kupingana
kisera ila baada ya chaguzi hakuna haja ya kuendelea kupingana ni
kuwa wamoja na kuwaletea wananchi maendeleo hivi hebu niulize ujenzi
huu wa barabara ya Lupingu ,Ludewa na Njombe Ludewa unaoendelea ni
kwa faida ya nani hii barabara inatumiwa na wana CCM pekee mbona
hata wapinzani mnapita katika barabara hiyo hiyo sasa
unapinga nini wakati huu wa CCM kutekeleza ilani yake ....tuwe na
uzalendo wa nchi yetu tusiwe wa kupinga kila kitu na mimi nikueleze
wazi kama ungejaribu kupinga mradi huu wa umeme kwa kutoshiriki
tungeonana wabaya mbele ya safari"
Akielezea
mradi huo wa umeme Filikunjombe alisema kuwa kwa kasi ambayo
wananchi wanaenda nayo katika kujitolea nguvu zao kuchimba mashimo
na kusogeza nguzo katika mashimo hayo ni
wazi mradi huo wa umeme utakamilika kabla ya Desemba mwaka huu .
Aidha
alisema kuwa wakati akiingia madarakani mwaka 2010 ni kijiji kimoja
pekee cha jimbo hilo la Ludewa ambacho kilikuwa na umeme wa mafuta
ila sasa zaidi ya vijiji 10 vina umeme na kuwa hadi sasa jumla ya
vijiji 49 vitafikiwa na mradi wa umeme huo ambao unatekelezwa kwa nguvu
za serikali ya Tanzania , Swedeni na kanisa na Romani Katoliki
Dayosisi ya Njombe.
|
No comments:
Post a Comment