Familia ya James Mwaisumbe ya Iringa na
Mbeya inapenda kuwashukuru wote walioshiriki mazishi ya mama yao
mpendwa na pia wale wote wanaoendelea kuelekeza maombi yao kwa
famili hii.
Ikumbukwe ni Tarehe 1/6/2013 ndipo
mpendwa wetu Grina James Mwaisumbe alipotutoka hapa duniani na sasa
kesho jumapili anafunga mwaka mmoja toka alipotutoka ,hivyo familia
inaendelea kumwombea na kumkumbuka kutokana na ucheshi wake na ukarim
na upendo mkubwa alioonyesha enzi za uwepo wake hapa duniani.
Grina anaendelea kukumbukwa na mume
wake mpendwa mchungaji James Mwaisumbe ,watoto Frank ,Mpeli
,Tukuswiga,Neema, Anna na wajukuu zako wote pamoja na ukoo wote wa
akina Mwaisumbe na Msika popote walipo.
Tunaendelea kuamini kuwa tulikupenda
sana na ulitupenda zaidi ila Mungu muweza wa yote amekupenda zaidi
yetu hivyo hatuna budi kuendelea kukuombea kwa Mungu .
Zaidi tutaendelea kuenzi yale yote uliyoonyesha enzi za uhai wake ikiwa ni pamoja na kuishi vema na watu .
Bwana alitoa na Bwana ametwaha jina lake na lihimidiwe milele Yote
Amina
No comments:
Post a Comment